Open-access Distribution, architectural design and functionality of megalithic structures of the Lake Eyasi Basin in northern Tanzania

Abstract

Tulitafiti miundo ya megalithiki katika Bonde la Ziwa Eyasi kaskazini mwa Tanzania ili kubaini asili ya mawe yaliyotumika katika ujenzi wake, kuelewa sababu za kuchagua mawe na mbinu za usafirishaji, pamoja na kutambua kundi au makundi ya watu waliohusika katika ujenzi wake. Matokeo yanaonyesha kuwa utamaduni wa megalithiki katika Bonde la Ziwa Eyasi ni ushahidi wa maendeleo ya kale ya kitamaduni, ubunifu, ustadi wa ufundi, na umuhimu wa kiimani. Megalithi hizi zipo za aina mbalimbali kama vile dolmeni, miduara ya mawe au mafuvu ya mazishi, na huonesha kutumika kama alama za kudumu za nyakati zilizopita. Huacha athari isiyofutika katika mandhari na katika uelewa wetu wa historia ya binadamu kwa kuchochea hisia ya udadisi kuhusu jamii zilizozijenga. Hivyo basi, ni dhahiri kwamba megalithiki katika bonde hili zinaonesha ujuzi wa hali ya juu wa uhandisi na kutoa mwanga juu ya vipengele vya kitamaduni, kijamii, na huenda vya kidini vya jamii zilizozijenga. Hata hivyo, madhumuni kamili ya ujenzi wake iwe ya kiroho, ya kiastronomia, au ya kumbukumbu pamoja na watu waliojenga, bado ni mada inayoendelea kujadiliwa na kuchunguzwa kitaaluma.

Lake Eyasi Basin; megalithic structures; pastoral Neolithic; Iron Age; megalithic builders


location_on
UJ Press 1 Jan Smuts Ave, Braamfontein, </br>Johannesburg, Gauteng, ZA, 2017, Tel: +27 11 717 6047 - E-mail: Matt.Lotter@wits.ac.za
rss_feed Acompañe los números de esta revista en su lector de RSS
Ir para arriba