Open-access Viashiria vya afya ya akili ya wanafunzi na umahiri wa kitaaluma

Abstract

Kukuza mafanikio ya kitaaluma na afya ya akili ya wanafunzi wa elimu ya juu kunaendelea kutambuliwa kama suala muhimu katika sekta ya elimu. Katika jitihada za kuandaa mikakati ya kukuza mafanikio ya wanafunzi na afya yao ya akili, seti ya takwimu iliyokuwepo ilichambuliwa upya iii kubaini viashiria vya umahiri wa kitaaluma na afya ya akili ya wanafunzi, kwa kutumia modeli ya kibaiosaikojamii kama mfumo wa nadharia. Takwimu za sehemu mtambuka zilizokusanywa kutoka kwa wanafunzi wa chuo kikuu (n=3,239) kupitia utafiti wa mtandaoni wakati wa janga la COVID-19 zilitumika. Uundaji wa milinganyo ya upimaji ulitumia maeneo mbalimbali ya ustawi (kimwili, kihisia, kijamii, kiroho, kifedha, kimazingira na kiakili) pamoja na matumaini, mbinu za kukabiliana na hali, na kuridhika na msaada wa taasisi iii kutabiri afya ya akili na umahiri wa kitaaluma (kama kiashirio mbadala cha mafanikio ya kitaaluma). Matumaini, uwezo wa kukabiliana, na umahiri wa kitaaluma vilikuwa viashiria vikuu vya moja kwa moja vya afya ya akili, pamoja na maeneo kadhaa ya ustawi (kiakili, kiroho na kihisia) kupitia uwezo wa kukabiliana kama kiungo cha upatanishi. Ustawi wa kiakili, uwezo wa kukabiliana, na kuridhika na msaada wa taasisi vilikuwa viashirio muhimu zaidi vya umahiri wa kitaaluma. Taasisi za elimu ya juu zinaweza kutumia matokeo haya kupanga rasilimali na huduma zinazofaa iii kukuza na kudumisha afya ya akili ya wanafunzi pamoja na utendaji wao wa kitaaluma.

Afya ya akili; umahiri wa kitaaluma; wanafunzi- wa elimu ya juu; huduma za msaada kwa wanafunzi; uundaji-wa mi!inganyo ya upimaji


location_on
Journal of Student Affairs in Africa 7 Walmer Road, Woodstock, Cape Town, Western Cape, ZA, 7925, Tel: +27 83 350 5959 - E-mail: editor@africanminds.co.za
rss_feed Stay informed of issues for this journal through your RSS reader
Go to top